Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imelikataa ombi la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao walikuwa wakiomba idhini ya mahakama hiyo iwaruhusu kumchukua mfanyabiashara Yusuf Manji kwa ajili ya kumhoji kuhusu masuala ya kodi.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkehe amesema endapo TRA wanahitaji kumhoji mtuhumiwa huyo, ni vyema wakatumia utaratibu mwingine itakayouona na si mahakama.

Aidha manji alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za uhujumu uchumi, kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18 mwaka huu itakapotajwa tena.

Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali.

 Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *