Staa wa Bollywood, Salman Khan ameachiliwa na mahakama nchini India kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mnyama wa mwituni aliye katika hatari ya kuangamia kabisa duniani.

Staa huyo alikuwa ameshtakiwa kosa la kuwaua swara watatu katika jimbo la Kaskazini la Rajasthan mwaka wa 1998 na mwaka uliopita aliachiliwa na mahakama kwa kosa jingine la kumkanyaga na kumuua mtu asiye na makazi.

Salman Khan, ni nyota wa filamu kutoka Bollywood, ambaye ana sifa ya kujikuta mashakani mara kwa mara.

Mwaka 1998 alilaumiwa na kabila moja la Rajasthan kwa kupiga risasi na kuwaua swara watatu wakati alipokuwa katika shughuli za uwindaji.

Salmani Khan amepatikana na kosa na mahakama ya chini na kuhukumiwa kifungo lakini sasa ameachiliwa huru baada ya kukata rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *