Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya kupewa dhamana kwa mfanyabiashara maarufu nchini Yusuf Manji.

Manji aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kupewa dhamana lakini imeshindikana na sasa amerejeshwa rumande.

 Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali.

Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *