Mahakama ya juu nchini Kenya itatoa uamuzi wa muda wa mwisho kuamua iwapo marejeleo ya uchaguzi wa urais yanaweza kufanyika siku ya Alhamisi.

Mahakama hiyo itasikiza ombi la dharura siku ya Jumatano kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafutiliwa mbali siku moja kablka ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Hatua hiyo inajiri baada bya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurejelewa.

Sasa inatakiwa kuingilia kati kwa mara nynegine na itaamua , ikiwa imesalia chini ya saa 24 kabla ya uchgauzi huo kufanyika kuhusu iwapo uchaguzoi huo unafaa kuendelea.

Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga ametumia mojawapo ya uamuzi wa mahakama kujiondoa katika uchaguzi huo akiutaja kuwa usio huru na haki na hautatoa maono ya Wakenya.

Rais aliyepo sasa Uhuru Kenyatta amesema kuwa uchaguzi huo ni sharti ufanyike, huku akiwa na muswada wa uchaguzi katika meza yake unaotarajiwa kutiwa saini

Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.

Inataka uchaguzi huo kubadilishwa na uchaguzi mpya hatua ambayo huenda ikaongeza muda wa uchaguzi huo kwa kipindi cha mwezi mmoja .

Wapiga kura watatu wameelekea katika mahakama ya juu wakitaka kusimamisha uchaguzi huo wa Alhamisi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *