Mahakama kuu kanda maalumu ya Iringa leo imeendelea na kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ’FFU’, Pasifius Simon.

Hukumu ya kesi hiyo awali ilipangwa kutolewa Julai 21 mwaka huu, iliahirishwa hadi leo kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa nje ya mkoa kikazi.

Mahakama kuu hiyo mkaoani Iringa imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia askari huyo na hivyo hukumu rasmi itatolewa siku ya jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *