Mahakama ya kikatiba nchini Afrika Kusini inatarajiwa kuamua kuhusu iwapo wabunge wanaweza kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma au la.

Hatua hiyo inajiri kufuatia hali ya sitofahamu kuhusu uongozi wa Rais Zuma huku kukiwa na madai ya uajiri wa marafiki zake serikalini na ufisadi.

Hivi karibuni Zuma alizomewa katika baadhi ya mikutano ya hadhara huku maafisa wakuu wa chama chake wakionekana hadharini kujipigia debe ili kumrithi kiongozi huyo kama kiongozi wa chama.

Upinzani unadai kwamba wabunge wanastahili kuongozwa imani yao na sio uongozi wa vyama vyao kwa kuwa uongozi wa rais Zuma ni swala muhimu la kitaifa.

Hatua hiyo ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye ilisababishwa na kumfuta kazi waziri wa fedha na naibu wake miezi miwili iliopita.

Hata hivyo baadhi ya wachanguzi wanaamini kwamba hata iwapo mahakama ya kikatiba itawapatia wabunge haki ya kupiga kura kwa siri, wanachama wengi wa ANC watamuunga mkono kiongozi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *