Naibu jaji mkuu nchi Kenya Philomena Mwilu, amesema kuwa kushindwa kwa IEBC kufuata agizo la mahakama kuhusu madai yaliyoibuliwa na upinzani, inaonyesha kuwa madai ya udukuzi yalikuwa ni ya ukweli.

Jaji Mwilu amesema mahakama ilikubaliana madai ya upinzani kuwa matokeo yalitangazwa kabla ya matokeo yote kutoka kwa vituo 40,000 kupokelewa.

Waangalizi walikosolewa vikali wakati uchaguzi ulifutwa kwa kuharakisha kusema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wenye uwazi.

Kwa upande wake jaji mkuu nchini Kenya David Maraga, amesema kuwa upinzani hakubaini madai yao kuwa kampeni za rais zilitumia fedha za umma kugharamia kampeni zao.

Jaji Maraga amesema kuwa sampuli kadha za fomu zilionyesha kuwa hazikuwa na mihuri rasmi, zingine hazikwa na sahihi na namba za usajili wala alama rasmi.

 

Amesema kuwa uchaguzi haukufutwa tu kwa sababu ulikuwa na hitilafu, lakini kile amekuwa akikichunguza ni ikiwa hitalafu hizo zilishawishi matokeo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *