Mashindano ya urembo ya idara ya magereza nchini Kenya yalifanyika wiki hii katika jela ya wanawake iliyoko Langata mjini Nairobi.

Washiriki huwa ni wanawake wafungwa pamoja na wale wako rumande, nia kubwa ikiwa ni kuwapa motisha na matumaini ya maisha.

Ruth Kamande aliibuka mshindi akifuatiwa na Tina Martin na Susan Wairimu akawa wa tatu. Wote hao wako rumande.

John Nene amezungumza na Ruth ambaye anakabiliwa na shtaka la mauaji na Tina kutoka Tanzania anayekabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *