Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo anatarajia kufanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.

Mahojiano hayo yatarushwa moja kwa moja na vituo vya habari vya redio na televisheni kutoka ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na yataanza saa 4:00 asubuhi.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imewaalika wananchi wote kusikiliza na kutazama mahojiano hayo ili mpate fursa ya kujua mambo mbalimbali ambayo Mheshimiwa Rais atayatolea majibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *