Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.

Katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi rais Magufuli amesema kuwa takriban shilingi bilioni 3.6 zimeokolewa kutokana na zoezi la kuwaondoa wanafunzi hewa kuanzia shule za msinngi hadi vyuo vikuu nchi nzima.

Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na namna ambavyo pesa za umma zinatumika kwa matumizi hewa kila mahali akitolea mfano wa wanafunzi hewa nchini ambao wamegundulika baada ya fedha za elimu bure kuanza kuingia mashuleni.

Rais ametolea mifano ya wanafunzi hewa katika mikoa ya Mwanza na kusema kuwa kuna wilaya ina wanafunzi hewa 5,000, Arusha kuna wilaya ina wanafunzi hewa 9,000 na Dar es Salaam 7,000.

Sambamba na hayo Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini kufanya uhakiki upya wa vyuo vikuu nchini ili kubaini ubora na vigezo vya wanafunzi wanaostahili kujiunga navyo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. Lwekaza Mundara amesema kuwa hosteli hizo zinazojengwa kwa shilingi bilioni 10 kutoka serikalini, zikikamilika zitasaidia kubeba wanafunzi takriban 3,840.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *