Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka TANESCO kuhakikisha linafikisha umeme wa uhakika mkoani Pwani katika eneo ambalo lililotengwa maalum kwa ajili ya viwanda.

Magufuli amezungumza leo Mkoani Pwani eneo la Mwandege wilayani Mkuranga, wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Azam.

Rais Magufuli amesema kuwa kati ya miundombinu muhimu katika uanzishwaji wa viwanda ni lazima kuwepo na umeme wa uhakika katika eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa ni jambo lisilovumilika kuona umeme haupatikani katika eneo hilo wakati miundombinu na kituo kikuu cha umeme kipo karibu na mkoa huo hivyo atachukua stahiki endapo watashindwa kufanya hivyo ndani ya muda wa miezi miwili.

Magufuli amesema kuwa katika kuwawezesha wawekezaji wenye nia njema atachukua mashamba makubwa yote ambayo hayajaendelezwa hata kama yanamilikiwa na waliowahi kuwa viongozi wa serikali ya Tanzania katika vipindi tofauti.

Pia Magufuli amewataka wawekezaji wazawa wajitokeze kwa wingi katika kuanzisha viwanda mbalimbali pamoja ili kukuza ajira kwa Watanzania pamoja na kulipa kodi ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *