Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation – DCI), Diwani Athuman Msuya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Rais Magufuli ametengua uteuzi huo leo.

Bila kutoa ufafanuzi wa sababu za mkuu huyo wa nchi kuchukua hatua hiyo, taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Athuman atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utatangazwa baadaye.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *