Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikienea katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba amezuia mziigo ya mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete.

Taarifa hizo zimekuwa zikidai taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), inayoongozwa na Mama Salma, imeshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoiingiza nchini Tanzania na hivyo kuwa hatarini kupigwa mnada.

Aidha, habari hizo zilikuwa zimedai Rais Magufuli anahusika kuzuia mizigo hiyo bandarini mpaka hapo itakapolipiwa kodi.

Taarifa ya ikulu imesema Rais Magufuli hajawahi kuzuia wala kuagiza kuzuiwa kwa mizigo ya Mama Salma.

Magufuli amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuacha kuandika na kuchapisha taarifa za uzushi na badala yake vizingatie weledi na kufuata sheria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *