Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli amesema chama hicho hakitambembeleza mtu kukichangia katika shughuli mbalimbali.

Akihutubia mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika leo Dodoma, Dk Magufuli amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kwa miaka yote CCM kimekuwa kikiomba hata kwa watu ambao hawastahili.

  “Matokeo yake wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kudhalilisha. Hakuna tena omba omba hatutaki kumbembeleza mtu akitaka kutuchangia atuchangie,”amesema.

Amesema kuwa chama hicho kina utajiri unaokiwezesha kujitegemea na kwamba mwanachama atakayetumia mali za chama kwa maslahi binafsi atachukuliwa hatua kali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *