Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo ameongoza waombolezaji na viongozi wa serikali na vyama vya siasa kuuaga mwili wa aliyekuwa Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.

Rais Magufuli amesema kuwa alimfahamu Dkt. Masaburi kama rafiki yake, ndugu yake, na mpiganaji mzuri wa Chama cha Mapinduzi, na kwamba ni mtu aliyefanya makubwa katika Jiji la Dar es Salaam.

Viongozi walioungana na Rais Magufuli katika kumuaga Masaburi ni pamoja na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Meya wa sasa wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Dk Masaburi ameaga dunia usiku wa kuamkia Alhamisi wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa akisumbuliwa na homa ya Ini (Hepatitis B).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *