Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama hicho hapo jana.

Kikao hicho kimefanyika Chamwino Mkoani Dodoma na kuhuduriwa na baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *