Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mabarawa kuwafukuza kazi mara moja watendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania(ATCL) watakaokwamisha ufanisi wa huduma za kampuni hiyo.

Rais Dkt Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa uzindizi wa ndege mpya mbili za ATCL aina ya Bombardier zilizonunuliwa kwa fedha taslimu za kodi za wananchi kutoka Canada.

Magufuli amesema shilingi Bilioni 100 zimetengwa kuanza ukarabati wa viwanja vya ndege nchini ili viweze kuhudumia ndege nyingi.

Pia Rais Magufuli amesema kuna mpango wa kununua ndege nyingine mbili moja yenye uwezo wa kubebea abiria 160 na nyingine watu 240.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *