Nchi ya Uturuki imevifungia kufanya kazi vyombo vya habari nchini humo, kufuatia jaribio la Mapinduzi lililoshindikana mapema mwezi huu.

Zaidi ya magazeti 45 na vituo 16 vya Televisheni vimeamriwa kufungwa kwa tuhuma za kuchochea mapinduzi hayo.

Tayari mamia ya watu wamewekwa kizuizini kwa kuhusisha na jaribio hilo la mapinduzi.

Viongozi wa upinzani kutoka vyama vya Republican na Nationalist wameelezea kuunga mkono hatua hiyo ya serikali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewataka maafisa wa Uturuki, kupeleka ushahidi haraka ili mahakama ziweze kutoa maamuzi ya kisheria haraka kwa watuhumiwa hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *