Aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga maarufu kama Ivan Don amezikwa jana nyumbani kwao Kayunga katika mji wa Kampala nchini Uganda.

Katika mazishi hayo magari ya kifahari yanayomilikiwa na matajiri wenzake wa nchini Uganda na Afrika Kusini.

Ivan aliyekuwa mume wa Zari alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kupata kiharusi na kuwa katika hali ya koma kwa wiki mbili mfululizo katika hospitali ya Steven Biko huko Pretoria nchini Afrika Kusini.

Miongoni mwa magari hayo ni pamoja na yale ya marehemu likiwemo Hammer lenye jina la Ivan 9, yale ya vizito mbalimbali wa jiji la Kampala waliohudhuria mazishi hayo pamoja na gari la tajiri wa Tanzania Jack Pemba aina ya Audi lenye jina la A Pemba ambalo lilionekana kuwa la kifahari zaidi.

Gari aina ya Udi linalomilikiwa natajiri wa kitanzania ambaye anaishi nchini Uganda, Jack Pemba.
Gari aina ya Udi linalomilikiwa na tajiri wa kitanzania ambaye anaishi nchini Uganda, Jack Pemba.

Katika hali ambayo haikuonekana kuwa ya kushangaza, baadhi ya waombolezaji walionekana wakiomba na kupewa fedha kutoka kwa matajiri mbalimbali waliohudhuria.

Hata hivyo kaburi la Ivan liliwekwa mafungu ya fedha chini ikiwa ni maandalizi ya kuuweka mwili wa bilionea huyo.

Mwili wa Ivan ambao uliwasili Uganda siku mbili zilizopita katika ndege kubwa iliyobeba watu 50, umezikwa katika makaburi ya familia pembeni ya kaburi la baba yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *