Vita vya maneno kati ya Nuh Mziwanda na ex wake Shilole haviishi.
Hata hivyo ni Nuh Mziwanda ndiye anayeonekana kuendelea kurusha makombora mengi zaidi kumzidi mwenzake.
Kwenye mahojiano na kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka, Nuh ameibuka na jingine kuwa kusema kuwa mafanikio aliyonayo sasa yanampa stress Shishi.
“Haamini ndani ya moyo wake ndio maana ameanza kupanick, lakini inabidi akubali matokeo kuwa mimi ni mwanamuziki na yeye ni mcheza show,” alisema Nuh.
Muimbaji huyo wa Jike Shupa amedai kuwa baada ya kuachana, Shilole aliamini kuwa maisha yatamwendekea kombo Nuh. Hata hivyo Nuh anasema anatamani ex wake huyo asingekuwa na kinyongo naye kwakuwa kila mmoja kwa sasa ana maisha yake na asiendelee kutaka kushindana naye.
Kwa upande mwingine, Nuh amesema girlfriend wake wa sasa ni wife material na atamuoa.
Tayari wawili hao wameshajichora tattoo za majina yao kuashiria kuwa wanapendana kwa dhati. Nuh amesema anadhani anaweza kuwa amempata ‘the one.’
“Kiukweli hapa nimefika,” alisema.
Nuh aliwahi kumvisha pete Shilole na kujichora tattoo ya jina lake ambayo hadi sasa anayo.