Mamia ya waandamanaji wamejitokeza katika miji mbali mbali nchini Marekani wakipinga ushindi wa Donald Trump kwenye uchaguzi mkuu.

Waandamanaji hao walikusanyika nje ya jumba kuu la Bw Trump, Trump Tower eneo la Manhattan jijini New York wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe “Not my president’ pamoja na mabango mengine.

Polisi hapo awali waliweka vizuizi vya saruji pamoja na kuchukua hatua nyingine za kiusalama nje ya jumba hilo refu linalopatikana barabara ya 5th Avenue jumba ambalo huenda likawa makao makuu ya Trump wakati wa kipindi cha mpito kabla yake kuingia White House.

hapendwi

Kuliripotiwa pia taarifa za waandamanaji kuziba lango la kuingia jumba la Trump Tower mjini Chicago siku ya jana huku wakiimba “No Trump, No KKK, No Fascists USA”  na “Not my president!”.

Miji iliyoongoza kwa maandamano hayo ni Oakland, California, na Portland, Oregon, waandamanaji waliteketeza bendera za Marekani kwa moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *