Madiwani watatu mkoani Kilimanjaro wamejiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM  kwa kile wanachodai kuwa ni kuweza kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewapokea madiwani hao watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM.

Madiwani waliojiuzulu ni, Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na  Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati.

Akizungumza wakati wa kutangaza azma hiyo, Goodluck Kimaro alisema kwamba CHADEMA hakuna demokrasia kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikijinasibu.

Akitolea mfano Halimashauri ya Wilaya ya Hai ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ni Mbunge wa jimbo hilo, alisema chama hakina uwezo wa kufanya jambo lolote dhidi ya mbunge.

Endapo mbunge atashindwa kutekeleza majukumu yake, chama ndio kinatakiwa kumuadhibu, lakini kwa upande wetu wa Hai hakuna uongozi wa kuweza kufanya hivyo.

Baada ya madiwani wote kuzungumza, Polepole alionya juu ya uwepo wa vitendo vya kihalifu kwa madiwani ambao wanahama CHADEMA na kusema jambo lolote likitokea kwa madiwani hao waliohama, watashughulikiwa ipasavyo na vyombo vya dola lakini pia chama hicho kingine ndio watakuwa wahusika.

Hadi sasa jumla ya madiwani 9 mkoani Arusha tayari wamejiunga na CCM na sasa watatu mkoani Kilimanjaro nao wamejiunga.

 

 

.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *