Madereva wa malori wa Tanzania waliotekwa na waasi wa kundi la Mai Mai katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambapo amesema madereva wote wapo salama.

Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka waasi hao.

Tukio hilo limetokea sehemu inayoitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *