Mwanamuziki wa Bongo fleva, Hamad Ali ‘Madee’  amesema kuwa iwapo angepata fursa ya kuwa kiongozi ndoto yake kubwa ilikuwa kuwaletea mandeleo watu wa Manzese.

Madee amesema kwa sasa Manzese imekua kutokana na kuongezeka kwa watu, hivyo ndoto yake kubwa ilikuwa kuwaletea huduma bora wakazi wa Manzese, pamoja na kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa vijana.

Madee aliendelea kusema kuwa anafurahishwa na serikali ya sasa kuwaacha vijana wa maeneo hayo kufanya biashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga, kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira na vijana kutoka maskani.

Madee amesema “Mwanzo walikuwa wanabughudhiwa sana lakini sasa hivi naona serikali imeaachia kwa sababu wameona ni vijana ambao hawataki kujihusisha na ukabaji, so naipa big up kwa hilo”.

Madee ni mwanamuziki wa aliyeanza muziki kitambo kama akiwa kiongozi anakuwa anafuata nyayo za wasanii wenzie walioingia kwenye siasa akiwepo Sugu pamoja na Profesa Jay.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *