Mkali wa Bongo fleva, Hamad Ally ‘Madee’ amesema kuwa meneja wake Babu Tale hakuitelekeza  Tip Top ila yupo karibu na Diamond Platnumz kutokana na mwanamuziki huyo kuwa na project nyingi.

Madee amesema hawezi kupinga maneno yaliyopo mtaani kwani ni kitu kinachoonekana kwao, lakini ukweli ni kwamba Babu Tale hajaitelekeza Tip Top, isipokuwa Diamond amekuwa na projects nyingi zinazohitaji uwepo wake kama meneja.

Hivi karibuni mashabiki wameibua hoja kuwa Babu Tale ameipotezea Tip Top na kugandana na Diamond, kwa sababu anafanya vizuri na safari za nje hazimuishi, kauli ambayo hata Niki Mbishi ameiimba kwenye wimbo wake wa Babu Talent.

Vile vile mwanamuziki wa hip hop, ROMA baadhi ya mstari wake kwenye wimbo wake mpya anasema ‘meneja kaikana Tip Top na kumganda Dangote’ akimaanisha kuwa Babu Tale kaikana Tip Top na kumganda Diamond.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *