Mtoto wa Mwl. Nyerere, Madaraka Nyerere amemtaka Diamond kuondoa picha ya Nyerere kwenye wimbo wake mpya ‘Acha Nikae Kimya’.

Hayo yamejiri baada ya malalamiko mengi toka kwa watanzania hasa watumiaji wa mtandao wa twitter kuwa Diamond ametumia isivyo picha ya mwalimu katika cover la wimbo wake mpya.

Madaraka ambaye ni mtoto mkubwa wa Hayati Nyerere amesema kuwa Mwalimu hakuwa mtu wa kukaa kimya hasa maovu yanapozidi alikuwa akikemea.

Juzi Diamond ameachia wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Acha Nikae Kimya’ akizungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii yanayoendelea nchini huku akiweka picha ya mwalimu Nyerere kwenye wimbo huo.

Baadhi ya watu wamekua wakiitafsiri tofauti wimbo huo kutokana na kubase kwenye masuala ya siasa wakati Diamond yeye ni mwanamuziki kwa hiyo anatakiwa kubaki kwenye njia yake ya muziki tu na si vinginevyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *