Shindano la kusaka vipaji vya kuimba nchini Bongo Star Search ‘BSS’ linatarajiwa kurejea tena nchini kama ilivyokuwa hapo awali.

Hayo yamethibitishwa na mwanzilishi wa shindano hilo Madam Rita wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio hapa nchini.

Madam Rita ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production ambao ni waandaaji wa shindano hilo linalosaka vipaji vya kuimba nchi nzima na kutoa zawadi ya mamilioni ya shilingi za Kitanzania kwa washindi.

Pia Madam Rita amesema kuwa wanajipanga kulifanya shindano hilo kuwa bora zaidi ili kuibua vipaji vya kweli kwa wasanii husika.

BSS ilipata umaarufu na kuibua vipaji kadhaa vya watu waliogeuka kuwa wasanii wakubwa nchini kama vile Kayumba Juma, Kala Jeremiah Baby Madaha.

Umaarufu wa shindano hilo pia ulitokana na majaji wake, Salama Jabir pamoja na wa tayarishaji wa muziki Master Jay (MJ Records) na P-Funk Majani (Bongo Records).

Mara ya mwisho, BSS ilifanyika mwaka 2015 ambapo Kayumba Juma aliibuka mshindi na kunyakua shilingi milioni hamsini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *