Madaktari nchini wamesitisha mgomo uliodumu kwa siku 100 baada ya kuafikiana na Serikali kuhusu nyongeza ya mishahara na maporesho sehemu ya kufanyia kazi.

Hii ni baada ya mgomo wa madaktari nchini kenya, ambao umedumu siku mia moja na kuathiri vibaya huduma za afya nchini humo.

Chama cha madaktari kikiongozwa na mwenyekiri wake Oroko Samuel, kuliungana na waziri wa Afya Cleopha Mailu kwenye ofisi za magavana wakati wa kutiwa sahihi makubaliano hayo.

Awali kulikuwa na hofu wakati madaktari walikataa kuingia ofisi ambapo makubaliano hayo yangetiwa sahihi, wakilalamikia utata wa vipengee fulani.

Madaktari walianza mgomo huo wakidai kuwa serikali imeshindwa kutimiza makubaliano waliyoafikiana, ya nyongeza ya mishahara yao na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya kazi.

Wiki iliyopita rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alitangaza kuwa madaktari wangechukuliwa hatua iwapo hawangemaliza mgomo wao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *