Mkali wa nyimbo ‘Muziki’ Darassa amesema kuwa madaktari wa hospitali ya taifa ya Muhimbili wamemshauri apumzike na apunguze mizunguko baada ya kuumia kichwa kutokana na ajali aliyoipata wiki iliyopita.

Darasa amesema baada ya kupata ajali alikuwa anasikia maumivu maeneo ya kichwani na kuamua kwenda kuangalia afya yake na kugundulika kupata itilafu ya kichwa kidogo ila kwasasa anaendelea vizuri.

Mkali amesema kuwa wamemcheki afya yake kwa sababu allikuwa anajisikia vibaya sana sehemu za kichwani lakini anashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa baada ya kupata damage ndogo.

Mwanamuziki huyo akiwa na muongozaji wa video nchini, Hanscana walipata ajali mbaya ya gari wakati wakiwa njiani wakitokea Kahama mkoani Shinyanga.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *