Mabaki ya ndege ya Burma iliyotoweka jana katika anga ya bahari ya Andaman ikiwa abiria 122 yamepatikana.

Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa iliyotolewa na idara ya jeshi nchini humo.

Ndege hiyo aina ya Y8, iliyotengezwa nchini China, ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.

Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa, wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano.

Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.

Mynmar imekumbwa na ajali kadha za ndege miaka ya hivi karibuni. Lakini ajali hii ya sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi, walifariki wakati ndege yao kuanguka kwenye mji mkuu wa Nay Pyi Taw.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *