Kiongozi wa upinzani nchini Gambia, Ousainou Darboe amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kutokana na makosa yanayohusiana na maandamano yaliyokuwa  yanaipinga Serikali ya nchi hiyo mwezi Aprili mwaka huu.

Kiongozi huyo amehukumiwa kifungo hiko pamoja wa watu 18 ambao pia walishiriki katika maandamano hayo nchini humo.

Bwana Darboe alishiriki maandamano hayo kulalamikia taarifa za kuuawa kwa mmoja wa viongozi wa chama chake, Solo Sandeng, akiwa kizuizini.

Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu lakini viongozi wa upinzani wanasema hautakuwa huru na wa haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *