Maelfu ya watu wameandamana usiku wa pili nchini Marekani kupinga ushindi wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ingawa hawakuwa wengi kama usiku wa kwanza.

Waandamanaji wengi wamekuwa vijana ambao wanasema uongozi wa Trump utazua

Akijibu maandamano hayo, Bw Trump ameandika kwenye ukarasa wake wa Twitter kwamba “si ya haki” yanayotendeka.

Waandamanaji walikusanyika katika miji mbalimbal Marekani kuanzia jana Alhamisi jioni wakipinga ushindi wa Donald Trump.

Polisi mjini Portland, Oregon wamesema maandamano hayo yanafaa kuchukuliwa kama ghasia kwasababu madirisha ya maduka yamevunjwa na baadhi ya waandamanaji walibeba magongo na mawe.

Mjini Philadelphia umati wa watu ulikusanyika nje ya ukumbi wa baraza la jiji na kuimba “Not Our President” (Si Rais Wetu), “Trans Against Trump” (Trans Dhidi ya Trump) na “Make America Safe For All” (Ifanye Marekani iwe Salama kwa Wote).

Mjini Baltimore, polisi wamesema watu 600 wameandamana kwa amani katika barabara za mji na kuzuia magari kupita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *