Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wafuasi wa chama hicho kulinda ofisi kuu ya Zanzibar dhidi ya uvamizi unaotarajiwa kufanyika.

Maalim Seif amesema amepata taarifa kuwa Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake wanajiandaa kuvamia makao makuu ya chama hicho Zanzibar.

Alitoa onyo kwa mtu yeyote ambaye atasogea kwenye makao makuu hayo kwa nia ya kufanya fujo, na kuwataka wanachama watiifu wa Zanzibar kuzilinda ofisi hizo.

Pia Maalim Seif alimshambulia mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Lipumba kwa kudai kuwavua madaraka wakurugenzi wa CUF Zanzibar na kuteua wakurugenzi wapya.

Akizungumza na wafuasi wake makao makuu ya CUF yaliopo Mtendeni, Maalim Seif alisema Prof. Lipumba hana mamlaka hayo kwani sio mwanachama tena wa chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *