Katibu mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad leo amefanya mkutano na wanachama wa chama hicho katika eneo ya Vuga kisiwani Unguja kwa ajili ya kuzungumzia mustakabali wa chama hicho.

Kwa upande mwingine, Mweneyekiti wa Chama hicho Prof. Lipumba nae anatarajiwa kufanya mkutano kwa ajili ya kuzungumza na wanachama na wafuasi wa CUF jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inakuja baada ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuandika barua inayomtambua Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho mpaka kupelekea wafuasi wake kukusanyika katika makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam.

Chama cha wananchi (CUF) kimekumbwa na mgogoro baada ya Lipumba kutaka kurejea katika nafasi yake kama mwenyekiti wa chama hicho baada ya kujiuzuru kabla ya uchaguzi mwaka jana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *