Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Seif Sharif Hamad jana Septemba ameenda jijini Nairobi nchini Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Lissu ambaye alipigwa risasi.

Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.

Taarifa hiyo ya Mtatiro ilisema kuwa “Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi”.

Maalim Seif ameongozana na Mhe. Juma Duni Haji Nairobi kumjulia hali, Mhe Tundu Lissu.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *