Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ameishutumu Wakala wa Usajili, Mufirisi na Udhamini (RITA) kwa kusajili Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CUF ambao anadai ni feki.

Maalim Seif amesema kuwa RITA imesajili wajumbe feki waliotangazwa na chama hicho upande wa mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba.

Katibu mkuu huyo amesema hayo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya RITA kusajili bodi ya wadhamini wiki iliyopita.

Amesema kuwa RITA imekiuka sheria kwa kusajirili bodi ya wadhamni ambayo ni feki haijulikani na wanachama wa chama hicho.

Kutokana na hayo Maalim Seif amesema kuwa watakwenda mahakamani kwa ajili ya kupinga usajili huyo uliofanywa na RITA kwa kudhamini bodi aliyoiita bodi feki.

Akijibu swali kuhusu mgawanyiko wa CUF ya upande wake na wa Lipumba, Maalim Seif amesema hakuna mgogoro wa CUF ya Lipimba na Maalim Seif bali ni mgogoro kati ya Lipumba na kundi lake dhidi ya chama hicho.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *