Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Hamad amekutana na kufanya mazungumzo na mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ofisini kwake Ubungo jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo walizungumzia mgogoro wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambao umekithiri kwasasa kutokana na pande mbili kuvutana.

Gwajima amesema kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ni rafiki yake hivyo alitaka kuonana naye ili aweze kujua Professa Ibrahim Lipumba anaharibu vipi chama.

Mchungaji Gwajima amesema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu huyo wa CUF na kusema aliamua kukutana na rafiki yake huyo ili ajue hilo baada ya hapo yeye atajua anafanyaje.

Kwa upande wake Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa amekaa na askofu Gwajima na kuzungumza naye kwa kina juu ya mgogoro huo wa Chama hicho.

Maalim Seif  amesema kuwa amemueleza mwenzake kile anachokifahamu na kusema ameamuchia askofu ili na yeye atafakari juu ya jambo hilo baada ya hapo anaamini huenda askofu akafanya jambo.

Baada ya mazungumzo hayo kumalizika Maalim Seif na msafara wake waliondoka Kanisani hapo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *