Ndege iliyokuwa imebeba Maofisa wa Umoja wa Ulaya (EU) imedondoka na kuwaka moto muda mchache baada ya kupaa katika Uwanja wa Ndege wa Malta huko Luqa majira ya saa 1.20 asubuhi leo.

Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano ambao wote wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ajali hiyo.

Harakati za uokoaji zinaendelea huku waokoaji wakisema uwezekano wa kukuta watu wakiwa hai ni mdogo sana.

Hakuna mtu yeyote aliyepona ndani ya ndege hiyo inayoelezwa kuwa ilikuwa ikitokea Misrata nchini Libya.

Waliofariki wanadhaniwa kuwa ni raia wa Ufaransa huku taarifa zikishindwa kueleza kama walikuwa ni maofisa wa usalama au raia wa kawaida.

Taarifa zinasema kuwa Ndege hiyo ilikuwa ni ya Shirika la ndege Frontex huku msemaji wa shirika hilo akikanusha kuwa ndege hiyo siyo ya shirika lao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *