Maafikiano kati ya serikali na jeshi yatimizwa Ivory Coast

0
213

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara amesema kuwa maafikiano yametimizwa ili kumaliza uhasama ndani ya jeshi la taifa hilo.

Ouattara, amesema kuwa wanajeshi waliokuwa wakishinikiza kulipwa marupurupu yao, watalipwa huku akiwaomba kurejea katika kambi zao.

Waziri wa ulinzi wa Ivory Coast, Alain-Richard Donwahi ambaye alikuwa amezuiliwa na wanajeshi hao ameachiwa huru.

Waziri huyo amekuwa akiendesha majadiliano katika mji wa Bouake, ulioko katikati mwa nchi hiyo, tangu siku ya Ijumaa.

Haijafahamika ikiwa wanajeshi hao wote, watakubali kuelewana na serikali.

.

 

LEAVE A REPLY