Kamanda mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa viongozi wastaafu wa jeshi la polisi hilo wamempa ushauri namna ambavyo anapaswa kuendesha jeshi hilo.

Sirro amesema kuwa viongozi hao wameona mapungufu mbalimbali ndani ya jeshi hilo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi.

Akiongea na waandishi wa habari IGP Sirro jana baada ya kumaliza mkutano na wastaafu hao alisema mambo kadhaa ambayo alishauriwa na viongozi hao ambayo jeshi la polisi linatakiwa kulifanyia kazi.

Baadhi ya maafisa wastaafu wa jeshi la polisi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na IGP Mstaafu Ernest Mangu, saidi Mwema, Omari Maita pamoja na makamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleman Kova na Afred Tibaigana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *