Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambao hawakamilisha zoezi la madawati kukamilsha utengenezaji huo ndani ya siku 14.

Waziri mkuu amesema kuwa kuwa wanafunzi watakapofungua shule, lazima wakae kwenye madawati hayo yaliyokamilika.

Majaliwa ameongeza kwa kusema kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi watakaoshindwa kutimiza agizo hilo hadi ifikapo Desemba 30 mwaka huu watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

Vile vile wakuu wa wilaya hayo na wakurugenzi wametakiwa kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza mwakani wanaanza masomo yao kwa awamu moja badala ya awamu mbili tofauti.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Arumeru katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *