Lyyn afungukia utajiri wake

0
167

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Irene Louis maarufu kama Lyyn amefunguka siri za utajiri wake kuwa ni mali alizoachiwa na wazazi wake na siyo kwamba amezipata kwa kudanga.

Mrembo huyo ambaye amekuwa akionekana kula bata kupita maelezo huku akiishi kwenye ghorofa la kifahari na kutembelea ndinga kali zaidi ya moja, aliendelea kueleza kwamba juhudi zake pia zimemfikisha hapo alipo, huku akipuuza uvumi kuwa amekuwa akiendesha maisha yake kwa kuhongwa na wanaume.

Mmoja kati ya mashabiki wake mtandaoni aliandika hivi karibuni kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Huyu Lyyn ni mdogo sana lakini anaishi maisha ya kifahari kama siyo kudanga huku ni nini?”

Mwanamuziki huyo ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tommy Flavour amekuwa akihusishwa na tabia za udangaji suala ambalo mwenyewe amelipinga vikali.

Kwasasa Lynn anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Maneno ambayo inaendelea kufanya vizuri katika media mbalimbali.

LEAVE A REPLY