Polisi nchini Zambia wamewakamata watu 133 wanaopinga kuchaguliwa tena kwa rais Edgar Lungu baada ya mpinzani wake mkubwa, Hakainde Hichilema kudai kuwa chama cha Lungu kiliiba kura.

Maandamano hayo yamezuka katika sehemu nyingi za mkoa wa Kusini ukiwemo mji maaarufu wa utaliinchini humo wa Livingstone.

Mkuu wa Polisi nchini Zambi, Godwin Phiri amesema kuwa waandamanaji walikuwa wakiwalenga wafuasi wa chama tawala na kisha kuharibu mali yao.

Bwana Hichilema amesema kuwa ana mpango wa kupeleka kesi mahakamani kupinga matokeo hayo yaliyomrudisha madarakani rais Lungu.

Rais Lungu ametangazwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata asilimia 50.35 kwenye uchaguzi huo huku Hichilema akipata asimia 47.67 ya kura zote katika uchagzui mkuu nchini humo uliofanyika siku ya Alhamis.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *