Upinzani nchini Zambia umeshutumu mamlaka ya uchaguzi kwa mipango ya kumpendelea Rais Edgar Lungu na kusema watapinga matokeo hayo katika Mahakama ya Katiba.

Rais wa Zambia, Edger Lungu jana ametangazwa kuwa mshindi licha ya malalamiko ya kutoka Chama cha upinzani kuhusu udanganyifu na wizi wa kura katika uchaguzi wa nchi hiyo.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema Rais Lungu amepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura akimshinda mpinzani wake Hakainde Hichilema ambaye amepata asilimia arobaini na nane ya kura zote.

Rais wa chama cha Movement for Multiparty Democracy, Dkt. Nevers Mumba amesema analo mkononi pingamizi la kuzuia matokeo yasitangazwe jambo ambalo lilipuuzwa na tume ya uchaguzi nchini humo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *