Muigizaji nyota wa Hollywood, Lupita Nyong’o amefunguka kufanyiwa unyanyasi wa kingono na mtayarishaji wa filamu nchini Marekani, Harvey Weinstein.

Lupita ambaye asili yake ni Mkenya ameeleza kuwa alifanyiwa vitendo hivyo akiwa chuoni akijaribu kutafuta nafasi ya uigizaji Hollywood.

Amesema kuwa alitambulishwa kwa Harvey na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mdau mkubwa wa filamu walipokutana katika hafla moja.

Lupita amesema kuwa mwanamke huyo alimwambia kuwa Harvey ni mtu muhimu sana kama anataka kufanikiwa kuigiza filamu kubwa zenye thamani ya mabilioni.

Lupita anasema baada ya siku kadhaa Harvey alimualika nyumbani kwake kwa lengo la kuangalia filamu lakini mambo hayakuwa kama alivyotarajia hapoa awali.

Lupita amesema kuwa “Nilikaa kwa ajili ya filamu, lakini baada ya dakika 15 Harvey alinifuata, aliniambia anataka kuniambia kitu. Alinipeleka hadi kwenye chumba chake cha kulala na akaniambia kuwa anataka kunipa ujumbe,”.

“Kwanza, nilidhani anatania. Lakini alikuwa hatanii. Kwa mara ya kwanza tangu nikutane naye nilijisikia siko salama. Nilipaniki kidogo na nikafikiria kitu cha haraka cha kumtuliza ambacho kitanifanya niweze kumdhibiti kutotumia nguvu,”.

“Alinikubalia, akalala kifudifudi na nikajifanya namtomasa mgongoni wakati naendelea kufikiria namponyoka vipi! Lakini kabla muda haujaenda aliniambia anataka kuvua nguo yake ya ndani. Nilimwambia asifanye hivyo kwa sababu sitaweza kuwa katika hali ya kawaida (confortable) hata kidogo. Hata hivyo, aliamka ili afanye hivyo. Na mimi niliamka na nikakimbilia kwenye mlango,”.

Lupita anasema kuwa Harvey alijaribu kumshawishi tena kwa kumtajia majina ya waigizaji wawili wa kike wakubwa wa Hollywood ambao wamefanikiwa sana baada ya kumliwaza kitandani.

“Nilimwambia siko tayari kufanya hivyo na kwamba kama hatuendi kuangalia filamu mimi narudi shule,”.

Harvey anakaririwa na kashfa za unyanyasaji wa kingono na kuwasumbua wanawake kingono kwa kutumia mgongo wa nafasi yake ya utayarishaji wa filamu katika kiwanda cha Hollywood.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *