Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amefika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili ya kusababisha kifo cha aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia.

Jana mahakamani hapo, Mdogo wa Kanumba, Seth alitoa ushahidi wake akiieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia ambapo Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo na Kanumba.

Leo mashahidi watatu wametoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika baada ya mashahidi hao kutoa ushahidi  na itaendelea kusikiliza ushahidi wa nne Oktoba 23 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *