Kesi  inayomkabili muigizaji maarufu wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhusishwa na kifo cha aSteven Kanumba imeanza kusikilizwa tena leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika, ushahidi upande wa Jamhuri ulitolewa na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco,  ambaye alikuwa shahidi wa kwanza.

Akijibu swali la wakili wa utetezi, Peter Kibatala, shahidi Seth ameieleza mahakama hiyo juu ya ugomvi alioushuhudia kati ya Elizabeth Michael na marehemu Steven Kanumba siku ya tukio.

Seth  ameieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia, uliosababishwa na simu kwamba, Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo.

Mbali na Seth, shahidi wa pili aliku,,wa ni daktari ambaye hata hivyo hakufika mahakamani hapo kwa kuwa aliomba udhuru kwa madai kuwa anaumwa. Jaji Rumanyika ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tatu. Mashahidi waliobaki ambao ni watatu watatoa ushahidi wao.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, mnamo Aprili 7, 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *