Baada ya muigizaji wa Bongo Movie, Dk. Cheni kusheherekea siku yake ya kuzaliwa muigizaji mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu’ amempongeza kufika siku hiyo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Lulu amemuandikia salamu za upendo na shukrani Muigizaji huyo kutokana na kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Lulu aliandika “Happy Birthday Baba…! Asante Kwa Kuwa Baba Mlezi Kwa Miaka Yote Tangu Uliponijua…..Asante Kwa Kuwa Mtu Wa Kwanza Uliyekiona Na Kukiamini Kipaji Changu Na Kuhakikisha Hakiishii Kwenye Macho yako Tu….Ninaweza Kusema Mpaka Hapa Nilipofika Kuna Mchango Wako Mkubwa sana…Mbali Na Wakati Wa Furaha Hujawahi Kuniacha Wala Kunikana Katika Shida Na Hata Aibu Zangu…..Sidhani Kama Kuna Kitu Naweza Kukulipa Wewe na Familia yako.

Pia ameongeza kwa kuandika “Unapoongeza Mwaka Mwingine Mungu wangu Ninayemuamini Akakuongeze Katika Kila Eneo…..Afya,Uzima,Maarifa,Uchumi na Akakutane Na Haja Zoooote Za Moyo Wako. @drchenitz @drchenitz @drchenitz”

Muigizaji huyo ameonesha hisia zake za upendo kwa muigizaji huyo mkongwe ambao wote walianzia katika kundi la maigizo la Kaole Sanaa Group.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *