Muigizaji nyota wa Bongo movie, Elizabeth Michael ‘Lulu ‘ amefunguka kwa kusema kuwa tangu alipopata tuzo ya AMVCA 2016 amekataa dili kadhaa kutoka kwa wasanii wa muziki nchini Nigeria.

Muigizaji huyo ameitaja sababu ya kukataa dili hizo imetokana na yeye si mwanamuziki wala video vixen kwa hiyo awezi kufanya kazi na wasanii hao wa muziki kutokana yeye anajishughulisha na uigizaji.

Elizabeth Michael (Lulu) ameshinda tuzo ya African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa nchini Nigeria akiwa na muigizaji mwenzie Single Mtambalike (Rich Rich).

Lulu ni muigizaji nyota wa Bongo movie ambaye ameanza kuigiza toka akiwa na umri mdogo akianzia katika kundi la Kaole Sanaa Group na kufanikiwa zaidi mpaka kupelekea kuchukua tuzo kubwa pamoja na kuingia mikataba na baadhi ya makampuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *