Muigizaji nyota wa Bongo movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa hakushiriki tuzo za EATV Awards kwa kwasababu hakufanya kazi kutokana na kuwa bize na masomo.

Lulu alipata nafasi ya kutoa tuzo ya  muigizaji bora wa kike kwenye tuzo za EATV zilizofanyika Mlimani City  mwaka huu.

Hata hivyo Lulu amesema kwa mwakani 2017 atakuwa nje ya masomo  hivyo mashabiki zake wategemee kazi nyingi zaidi kutoka kwake na vitu mbalimbali ili kuweza kuwaridhisha mashabiki zake ambao walimkosa kwa muda wa mwaka mzima akiwa masomoni.

Pia Lulu hakusita kutoa pongezi kwa waandaaji wa EATV AWARD mwaka 2016 kwa kuandaa tuzo hizo lakini pia kwa kumpa nafasi ya kuweza kutoa tuzo ya muigizaji bora wa kike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *